Wafanyi biashara wa soko la bushili lililo katika wadi ya ingotse-matiha eneo bunge la navakholo kaunti ya kakamega wanaiomba serikali ya kaunti usaidizi wa kuimarisha soko hilo ambalo wanasema wamebaki nyuma kimaendeleo.

Wanalilia swala la maji na vyoo na ujenzi wa vibanda vya kuuzia ambapo wanasema kwamba licha ya wao kutoa ushuru, bado wanahangaika kila wakija sokoni.


“Hatuna ata choo hakuna maji sasa hii ni soko gani. Soko zingine zimejegwa ziko na choo ziko na maji na pia ziko na mwangaza. Tunalipanga ushuru kila siku hatujui hiyo pesa hufanya nini haswa serikali ya kaunti mwangazie hii maneno”

Hata hivyo wameipongeza serikali ya kaunti kwa kuwaletea mnara wa taa kwenye soko hilo.

By Wickliffe Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE