Hali ya simanzi imetanda katika maeneo ya Lubao wakati wa kuwasilishwa kwa mwili wa mwenda-zake Agnes Isiako katika parokia ya Familia Takatifu Lubao aliyekuwa mwana kwaya maarufu.

Ni msafara ulioshuhudiwa ukisindikizwa na magari aina ya tuktuk zaidi ya thelathini na tatu, pikipiki ishirini na sita, basi moja na magari ndogo kumi na tano.

Hata hivyo padre mkuu wa parokia hiyo  Ken Lwile,      alisimama kidede na kutoa agizo la kuzingatia masharti ya covid-19 ambapo ni watu wachache waliruhusiwa kuingia kanisani

Ibaada ya mazishi itafanyika kesho jumamosi 10-04-2021 chini ya masharti ya covid-19, ikiongozwa na kanisa katoliki nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Kibung’aya, lokesheni ndogo ya Indangalasia, lokesheni ya Shikoti katika wadi ya Butsotso Mashariki kaunti ndogo ya Lurhambi kaunti ya Kakamega.

By sajida Wycliffe

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE