Hali ya simanzi imekubika kijiji cha Ebukhubalo, Butonga kwenye kata ya Lusumu eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega baada ya mwanafunzi msichana wa kidato cha kwanza shule ya upili ya Butonga kupatikana amejitia kitanzi kwa nyumba ya ndugu yake mapema leo.

Kulingana na wazazi wake wanasema Norah Makokha mwenye miaka 19 aliamka asubuhi vyema wala hakuzozona au kukosana na yeyote kabla ya kifo chake

 “Mtoto wangu amekufa kwa njia ata atuelewi, serikali tusaidie tujue ni nini imesababisha kifo chake. huyu mtoto akukua amekosana na mtu yeyote sasa atujui ni nini inamefanya akakufa”

Akidhibitisha kisa hiki naibu wa chifu wa Butonga Peter Naviswa amesema kuwa mtoto huyo huenda alichukuwa hatua hiyo kutokana na kuwepo kutoelewa na aliyempachika mimba

 Huyu msichana amejinyongea kwa nyumba ya ndugu yake. tumeangalia simu ambayo amekua nayo tukapata message ni kama alikua amegombana na boyfiend hata tumeona message ambayo amemtumia akisema “leo ni siku ya mwisho umeniona na utai niona tena. amekua ni mwanafunzi wa kidato cha kwanaza shule ya upili ya Butonga. 

Mwili wa mwendazake ulichukuliwa na maafisa wa  polisi wa Navakholo na kupelekwa kwenye hifadhi ya miili ya wafu ya rufaa ya Kakamega.

By Ernest Luvisia

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE