Wachuuzi mjini Kakamega wamebaki vinywa wazi baada ya kushuhudia kisa cha mwanamume mmoja mwenye umri wa kadri kula nyasi kwa tuhuma za wizi.
Kulingana na wachuuzi walioshuhudia kisa hicho wakiongozwa na Peter Nyatukai wamesema huenda jamaa huyo ambaye pia ni mchuuzi mjini humo alikuwa amemwibia mchuuzi mmoja mali yake kabla ya kuandamwa na mazingaubwe hayo.
Hata hivyo vijana kaunti hiyo wameshauriwa kutotumia njia za mkato kujitajirisha badala yake wajitafutie mali kwa njia halisi.
By Richard Milimu