Siku chache baada ya waziri wa kilimo Peter Munya kutangaza kuongeza bei ya miwa ya shilingi elfu nne na mia mbili kwa kila tani , baadhi ya wakulima kutoka kaunti ya Kakamega wamepongeza hatua hiyo japo wametaka malipo hayo mapya kuwekwa kuwa sheria.

Wakiongozwa na George Kawa wakulima hao wamepongeza hatua hiyo ila wanasema kuwa tangazo hilo litatimizwa na kampuni kusiaga sukari  uwapo waziri ataifanya kuwa sheria.

Wakati uo huokawa amemtaka waziri Munya kuwaondoa madalali wanaowanyanyasa wakulima kwa kununua miwa zao kwa bei ya chini na kuuzia kampuni za kusiaga sukari kwa bei ya juu kwani wamechangia pakubwa wakulima wengi kushindwa kuvuna miwa yao na kupata hasara.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE