Mwanaume mmoja wa miaka ya makamo kutoka kijiji cha Shihunga kata ndogo ya shirembe eneo bunge la Butere kaunti ya Kakamega anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Butere baada ya kupokea kichapo cha mbwa na kunusurika kifo alipofumaniwa akila uroda na mke wa mwanawe majira ya usiku.

Kulingana na  familia wakiongozwa na Agrrey Njomo wanasema kuwa wawili hao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kwani bwana wa mwanamke huyo anafanya kazi maeneo ya Nakuru na walitumia fursa hiyo kushiriki mapenzi usiku kwenye nyumba ya mwanamke huyo kabla ya kufamaniwa.

Kijana amepatinana pale akiwa ametoa viatu na nilipo ingia kwa nyumba na akaingia chini ya kitanda na nikawatoa nikafunga mlango na nikaita chifu akuje kuangalia hiyo maneno

 Familia hiyo imeongeza kuwa juhudi zao za kuwakalisha chini na hata kuwapeleka kwenye baraza ya wazee kuwatenganisha hazijafua dafu kwani wameendelea na uhusiano huo wa kimapenzi ikizingitiwa kuwa ni baba mkwe na mkaza mwana.

Huyu ni baba mkwe wake lakini sasa ni wapi mambo kama haya inafanyika hii ni tabia ambayo sijaweai sikia tangu nizaliwe na leo imepatikana na imekua wazi kwamba ni uhusiano wamekua nayo tangu kitambo

Watawala wa sehemu hiyo wakiongozwa na mzee wa mtaa Enock Sande ambao wameshtumu kitendo hicho wamehoji kuwa wawili hao wamewashangaza wengi wakisema kuwa hiyo ni kuleta laana katika familia.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE