Familia moja kutoka kijiji cha Kiptii, wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon imetoa wito wa wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwapa usaidizi wa kifedha ili kumudu gharama ya matibabu ya mwanawe mwenye changamoto ya neva( nerves complications) hali ambayo imemlemaza miguu yote miwili.

Kulingana na Silas Ngeywo ambaye ni babake mtoto huyo  Abigael Chebet mwenye umri wa miaka sita amepitia hali ngumu baada ya kukosa fedha,  za kugharamia matibabu ya mwanawe ambaye amelemaa miguu yote na kutoa wito kwa wahisani pamoja na viongozi wa eneo hilo, kumpa msaada wa dharura semi zilizotiliwa mkazo na mamake marion nelima.

Aidha Ngeywo amedokeza kuwa amefanya kila juhudi  kumtafutia mwanawe  matibabu ambaye amekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya tuikut kabla ya kukumbwa na shida hiyo mwaka jana, kwenye hospitali za eneo hilo bila mafanikio na alilemewa na gharama ya matibabu wakati  akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa mjini Bungoma.

Na cha kuhuzunisha zaidi ni kuwa familia hiyo bado inaomboleza kifo cha mwanawe aliyeaga dunia na kuzikwa hivi maajuzi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE