Mamia ya watumizi wa barabara ya Shianda kuelekea Malaa na ile ya Eluche kuelekea Mung’ang’a katika eneo bunge la Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega wameandamana kulalamikia hali mbaya ya barabara hizo

Wakaazi hao wenye hamaki walipanda migomba ya ndizi na miwa kwenye barabara hizo, wahudumu wa bodaboda wakilalamikia kupata hasara haswa kunaponyesha wakielekeza gadhabu yao kwa mbunge wao Benjamin Washiali.

Mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali japo amesikitikia mahangaiko ya wakaazi amejitenga na shutuma hizo akisema ujenzi wa barabara hizo unashughulikia na shirika la Kera na wala sio afisi yake

Ujenzi wa barabra ya kutoka Shianda kuelekea Navakholo ulizinduliwa na rais Uhuru Kenyataa mwaka wa 2016 na hadi kufikia sasa ujenzi huo haujakamilika mwanakandarasia asijulikana aliko.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE