Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amesema BBI ndio itaweza kuwezesha maeneo yote ya nchi kupata maendeleo akiongeza kuwa maendeleo vijana na watu wa kike ndio watanufaika pakubwa iwapo watakubali kupitisha BBI.

Raila aliyasema haya akiwa katika mazishi ya mama Selina Nasike mamake gavana wa kaunti ya Bungoma Wyclife Wangamati yalioandaliwa katika uwanja wa ndege wa Bungoma leo.

Aidha Raila alipuzilia mbali mapendekezo ya naibu wa rais William Ruto ya kuwapa vijana nchini wheelbarrow akisema aahadi aliyoitoa kwa wakenya ya kutengeneza nafasi za kazi hadi kufikia sasa ni ndoto.

“Wengine huko mbeleni waliahidi watazalisha kazi ya milioni moja kwa mwaka. Waliahidi vijana chini ya miezi sita watapata laptop lakini hatujaona na sasa wako katika darasa la nane. Tunataka tupitishe BBI kwamaana ni dhahabu tena almasi ambayo itasaidia akina mama pamoja na vijana.”

Vile vile Raila aliwapongeza wawakilishi wadi wa kaunti zilizopitisha BBI akiwataka wakenya kuiunga mkono watakapohitajika kuipigia kura ya maoni.

“Natoa shukrani kwa MCAs wote ambao wamepitisha BBI na rais alisema ataleta kaunti zote za Mt Kenya na mimi nikamwambia nitaleta kaunti zote za nyanza na western na sasa super tusday BBI si ilipita?”alisema Raila

Naye Spika wa bunge la Seneti Ken Lusaka alithibitisha kuwa bunge tayari limepokea miswada ilipitishwa kutoka kwa kaunti kadhaa nchini tayari kuanza kuzishughulikia kwa mujibu wa sheria

“I want to conferm that we have resived 32 copies out of the all counties in the parliament na nahakikishia wakenya kwamba tutafata katiba na kuelekeza wakenya kwa njia mwafaka hadi watakapo piga kura.” Alisema Spika Lusaka

Naye Eugine Wamalwa waziri wa ugatuzi alipuzilia mbali wale wanaosema serikali haina uwezo wa kupeana asilimia 35 kwa kaunti kuwa wanaeneza uongo akiongeza kuwa Serikali haijawahi kosa kutoa pesa zote kwa kaunti tangu mfumo wa ugatuzi uanze nchini.

Story by Imelda Lihavi

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE