Kanisa la PAG Kenya limewataka wanasiasa kupunguza joto la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa kwa sasa na badala yake kushirikiana na kanisa kuhubiri amani .
Akizungumza kwenye ibaada ya jumapili katika kanisa la Makale PAG eneo bunge la Malava , askofu mkuu mwangalizi wa kanisa hilo nchini kasisi Patrick Lihanda amekashifu joto hilo linaloendelezwa na wanasiasa yakiwemo matamshi ya kuvuruga amani huku akihoji kuwa huenda matamshi hayo ndio yanayosababisha utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi shuleni.
Wakati huo uo askofu huyo amewataka wanaopigia debe mchakato wa BBI ,kuhusisha viongozi wengine likiwemo kanisa pasina kuwalazimisha wakenya kuiunga mkono.
Ni kauli iliyotiliwa mkazo na askofu wa kanisa hilo maeneo ya malava Joseph Masache ambaye ametaka nakala za BBI kusambazwa mashinani ili wakenya waweze kujisomea na kuelewa yaliyomo.
Story by Imelda Lihavi