Lubao FM | 102.2 Hz

Malori 150 ya mahindi kukwama Bohari

 Hali si hali kwa wakulima kutoka kaunti ua Uasin Gishu baada ya malori 150 za mahindi kukwama Bohari(warehouse) baada ya bei ya mahindi kupunguzwa ghafula kutoka shilingi elfu mbili mia saba hadi elfu mbili mia tano na hamsini bila kuwapa ilani yeyote.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa idara ya kilimo na mifugo na mbunge wa eneo la bunge la Moiben Silas Tiren akihutubia waandishi wa habari amekashifu vikali bodi inayohusika kwa kosa la kutohusisha wakulima wanapopandisha bei ya mahindi bila kuwapa ilani ya mwezi moja.

“watu waleta mahindi yao wakati mmepima ndio mnawambia mmepunguza bei ya mahindi kutoka 2700 hadi 2500, na mulikubalina na akina nani kwa hiyo bei. Bodi ifanye petition na wakulima waweze kuelewana.”

Hata hivyo Tiren ametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta na waziri wa kilimo Peter Munya kuingilia kati na kutafuta suluhu ya kudumu kwani kuna mabwenyenye wanaojaribu kuwanyanyasa wakulima.

Mkurugenzi wa chama cha wakulima Kipkorir Arap Menjo amesema kuwa wanafaa kuwa na sheria za mabohari ( warehouse) ambapo shirika zingine zinapoungana na wakulima zinafaa kufuata kanuni hizo.

Vile vile wakulima wametoa wito kwa serikali kuingilia na kuwacha kupuuza maslahi yao kwani bei ya mbolea ilipanda hadi 3200 na 

imewathiri pakubwa.

Story by Sharon Lukorito

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE