Wazazi wanashauriwa kukaa na wanao kwa njia nzuri wakiwemo wa darasa la nane na wa kidato cha nne wanapojiandaa kuukalia mtihani wa kitaifa mwezi machi mwaka huu.

Akiwahutubia waombolezaji katika ibaada ya mazishi ya mwenda zake solomon mushila shabola, katika kijiji cha bukhaywa wadi ya isukha kaskazini eneo bunge la shinyalu kaunti ya kakamega hii leo, mwakilishi wadi wa isukha kaskazini hellemina lanziva anawaomba wazazi kuwasaidia wanao kwa njia nzuri ili kufanya vema katika mtihani wao shuleni.

Mwakilishi huyo anawaomba wakaazi kuipigia kura na kuipitisha nakala ya b.b.i kwani inayo mambo mazuri kwa mwananchi.

Kwa upande wake naibu chifu wa kata ndogo ya lubao ambaye pia ni kaimu naibu chifu kata ndogo ya buyangu suluvey ashiono, anawauliza wale wanahitaji kujiunga na masomo ya ualimu kwenye kiwango cha p1 kuenda kujisajili kwenye kaunti.

Kuhusu huduma namba naibu chifu anawauliza wakaazi wa ileho kuenda kuichukua kadi zao katika afisi za d.o kambiri huku wakaazi wa  shinyalu nao waende katika afisi za d.c kuanzia 01-03 -2021.

Ni ibaada iliyohudhuriwa na wakurugenzi wa kituo hiki cha 102.2 lubao fm ili kuwafariji jamii ya mwenda zake kwa kuwatia moyo na kuzitangaza baadhi ya vipindi vinavyoendeshwa katika kituo hiki.

story by Sajida Wycliffe

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE