Wito umetolewa kwa waziri wa fedha Ukur Yattani kuzingatia kupunguza bei ya mafuta na bidhaa za mafuta ya petroli anapotarajiwa kesho kusoma makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2021/22.
Askofu Ignatius Wanjala wa kanisa la Revival Living Ministries mjini Bungoma amesema bei ya mafuta imeathiri pakubwa uchumi hasa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Wakati uo huo, Wanjala ameiomba serikali kupitia wizara ya elimu kuwapa wazazi muda zaidi ili kukamilisha malipo ya karo ya wanao shuleni.
Amesema amri ya waziri wa elimu Profesa George Magoha kuwa wazazi walipe karo huenda ikawa mzigo kwa wazazi wengi nchini.
Haya yanajiri huku baadhi ya wabungewakiteta kuhusu kucheleweshwa kwa fedha za kufadhili maendeleo katika maeneo bunge almaarufu kama CDF.
By Hillary Karungani