Waziri wa Kilimo Peter Munya amemteua Dakt Chrispinus Ogutu katika wadhifa wa Kaimu Meneja wa kiwanda cha sukari cha Nzoia baada ya aliyekuwa meneja wa kiwanda hicho Wanjala Makokha kusimamishwa kwa kipindi cha miezi mitatu huku uchunguzi ukianzishwa dhiti yake kuhusu madai ya ufisadi.

Akitoa taarifa hiyo, Katibu mtendaji katika wizara ya kilimo Lawrence Omuhaka amesema mabadiliko hayo yanaanza kutekelezwa mara moja huku kamati maalum ikibuniwa kuanzisha uchunguzi katika madai ya ufisadi yanayomkabili meneja anayeondoka.

Baadhi ya sababu ambazo zimetajwa kuchangia kutimuliwa kwa meneja anayeondoka  ni pamoja na madeni ya wakulima ya zaidi ya miezi saba, utoaji zabuni kinyume cha taratibu za sheria, kukosa kufanyia marekebisho mashine za kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka sita na wafanyakazi kukosa kulipwa mishahara yao.

Haya yanajiri huku utata kuhusu jinsi ya kufufua kiwanda cha sukari cha Mumias katika Kaunti ya Kakamega ukiendelea. 

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE