Zaidi ya wakazi 2000 wa wadi ya Ingotse-Matiha eneo bunge la Navakholo wataanza kupokea maji safi ya mfereji baada ya mradi wa Obulamu Community Water Project kuzinduliwa rasmi katika eneo la Ingotse.

Wenyeji wanasema wamepitia shida si haba kabla na ni afueni kwao kupata maji safi kupitia kwa mradi huu

Mradi huo unaotumia miale ya jua ulifadhiliwa na jamii, serikali ya kaunti Kakamega na kampuni ya maji ya Davis & Shirtliff unalenga kutoa maji kwa wakazi wapatao 2000 jinsi anavyoelezea Loice Mutua meneja wa kampuni hio tawi la Kakamega. 

Afisa mkuu wa idara ya maji na mazingira kwenye kaunti ya Kakamega Joseck Maloba akizungumza kwenye hafla hio anasema changamoto wanayokumbana nayo ni uharibifu wa vifaa vya miradi ambapo ametoa wito kwa ushirikiano. 

Waanzilishi wa mradi huu wakiongozwa na Isaac Litali chifu wa eneo hilo Wyclife Kombo na James Kasiamani  wamewataka watakaonufaika na mradi huu kukuumbatia ili kunufaisha kizazi kijacho

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE