Wakulima wa kahawa katika chama cha ushirika cha Sibumba eneobunge la Sirisia wamejitokeza kushiriki zoezi la kuwachagua viongozi watakaosimamia chama hicho kwa muhula wa miaka mitatu.
Wakizungumza baada ya kushiriki zoezi hilo viongozi waliochaguliwa kuwakilisha maeneo mbalimbali wamewapongeza wakulima kwa kuwapa nafasi hiyo huku wakiahidi kuchapa kazi kando na kulinda mazao ya mkulima.
Baadhi ya wagombezi walioshiriki kinyang’anyiro hicho pasi na kufaulu walielezea kutoridhishwa kwao na zoezi hilo, huku wakiomba kurejelewa kwa zoezi hilo katika baadhi ya maeneo wakidai kuwa zoezi hilo lilikumbwa na changamoto si haba.
Hata hivyo mkurugenzi wa vyama vya ushirika eneobunge la Sirisia Pius Mbai amewataka wawaniaji viti mbalimbali ambao hawakuridhika na matokeo hayo kuwasilisha lalama zao kwa kufwata sheria.
By Richard Milimu