Watu wanaoishi na changamoto za ulemavu eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega wameitaka wizara inashughulikia maswala ya walemavu nchini kuweka mikakati ya kusafisha sajili ya watu hao kama njia mojawapo ya kupata idadi kamili ya watu wanaoishi na ulemavu na kuziba mianya ya ufujaji wa pesa ambazo zimetengewa kuwafadhili

Ni kauli yake mwanaharakati wa kutetea haki za watu wanaoishi na ulemavu eneo bunge la Navakholo kaunti  ya Kakamega Barthez Wechuli, ambaye anasema tangu kubuniwa kwa sajili hiyo hadi sasa haijawahi safishwa huku wengi wa walemavu wakitatizika licha ya baadhi ya watu ambao walisajiliwa mwanzoni kunufaika kwa mpango wa serikali wa kuinua jamii kuaga dunia

Wechuli kadhalika ameitaka wizara ya fedha kwa ushirikiano na wizara ya elimu kutenga mgao toshelezi wa kushughulikia mahitaji maalum ya watoto wanaoishi na ulemavu na pia kuajiri walimu zaidi wa kuwasaidia watoto hao mbali na kuwepo kwa mikakati ya kuwawezesha kupata fedha za kuwasaidia kuendesha biashara

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE