Mwanasiasa David Wamatsi amekanusha tetesi kuwa Chama Cha ANC kinapinga ufufuzi wa kiwanda cha sukari Cha MUMIAS
Akizungumza nyumbani kwake kwenye hafla ya ukumbusho wa marehemu mamake Jesicah Omusotsi mwanasiasa huyo amewataka wanasiasa kukoma kutumia swala la MUMIAS kujinufaisha kisiasa
Amewataka wakaazi kujiandikisha kwa wingi kama wanachama wa ANC ili kukipa Chama hicho umaarufu kote nchini
Mwaniaji huyo wa kiti Cha ubunge eneobunge la MUMIAS Mashariki amewataka wakaazi kumuunga mkono Musalia Mudavadi ili kunufaika na miradi ya maendeleo huku akimsuta naiburais akimtaja kama asiye na lolote jipya kwa jamii ya Mulembe
By James Nadwa