Mbunge wa Sirisia John Koyi Waluke amewashauri vijana kujiunga na chuo cha kiufundi cha Sirisia ili kupata ujuzi na maarifa itakayowawezesha kujikimu siku za usoni.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi ya Bi Priscillah Nasambu Wamasi katika kijiji cha Chongoyi eneobunge la Sirisia, waluke amesikitikia idadi ndogo ya wanafunzi waliojisajili kwenye chuo hicho huku akiwataka wazazi kuwalipia wanano karo itakayowawezesha kujiendeleza kimasomo.

Mwakilishi wadi ya Bukembe Mashariki katika bunge la kaunti ya Bungoma Joram Wanyonyi na mwahaharakati wa kisiasa kaunti hii Simiyu Mutaki wakimtaka mwakilishi wadi ya Lwandanyi Tony Barasa kuwapa heshima ya kutosha viongozi walio mamlakani.

Kwenye hafla hiyo ya mazishi gavana wa kaunti hii Wycliffe Wangamati alidokeza kuwa zaidi ya wanafunzi elfu moja na mia tano werevu kutoka jamii masikini watanufaika na mpango wa governor’s scholarship utakaowawezesha kuendelea na masomo yao.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE