Boda boda eneo bunge la Nambale kaunti ya Busia wamelalamikia kile walichokidai kuwa  kuhangaishwa na maafisa wa kushika doria kabla ya masaa ya curfew kuanza,

Wakizungumza na wanahabari mjini Nambale boda boda hao wamedai kuwa  hawaja kaidi amri ya Rais Uhuru Kenyatta ya kufunga kazi saa moja ila wameshangaa na kitendo cha kuandamwa na maafisa ya usalama kabla ya saa mbili usiku,

Hivyo basi wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Busia kupitia gavana wa gatuzi hilo Sospeter Ojamong kuingilia kati ili kuwanusuru na kero hilo,

Ikumbukwe kuwa wiki chache zilizopita Rais Uhuru Kenyatta  aliziwekea vikwazo  takribani kaunti kumi na tatu za ukanda huu  za  kutotoka nje baada ya saa moja jioni amri ambayo imepokelewa na hisia mseto kutoka kwa watu wa tabaka mbali mbali

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE