Kumekuwa na shamrashamra kubwa katika maeneo mbalimbali ya England kufuatia timu ya taifa hilo kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Euro 2020
England iliwachabanga Denmark 2-1 na kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza na fainali yake ya kwanza ya michuano mikubwa katika miaka 55 iliyopita
Mara ya mwisho taifa hilo kufuzu fainali katika soka la wanaume ilikuwa mwaka 1966 ilipotwaa kombe la dunia.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alianza kuongoza sherehe hizo toka jana akiwa na mkewe Carrie, huku video kadhaa zinazosambaa mtandaoni zikionyesha mashabiki wa timu hiyo wakiimba na kutamba kwamba kombe la Euro mwaka huu linaenda nyumbani kwa maana ya England.
Huko Newcastle, polisi walilazimika kuwatawanya baadhi ya mashabiki waliokuwa wanakesha usiku kucha kushangilia ushindi huo katika maeneo yaliyo karibu na Central Station Sifa kubwa ya England ni kuwa na Mashabiki wengi wanaopenda sana soka na wanafuatilia vilabu vyao na kuunga mkono timu yao ya taifa
Getty Getty Images
Katika majiji ya London, Liverpool, Manchester na Stoke pia shangwe zilikuwa kubwa, mashabiki wakionekana
kuvua mashati na wengine wakinywa pombe kama ishara ya furaha yao ya ushindi
Wengi wamepongeza hatua iliyofikia timu hiyo akiwemo nahodha wa zamani wa England, Wayne Rooney aliyechapisha picha katika mtandao wake wa twitter, akiwa na familia yake kufurahia matokeo ya usiku wa jana.
By Samson Nyongesa