Wakizungumza na wanahabari nje ya ofisi za usajili wa vyeti hivyo mjini Bungoma,wakaazi hao wakiongozwa na Hillary Barasa wamesema kuwa wamechoshwa na ahadi za kila siku, huku wakitumia nauli kusafiri kutoka mbali kwa minajili ya shughuli hiyo.
Aidha Barasa pia ametoa wito kwa viongozi eneo laBungoma akiwemo kamishna wa Kaunti ya Bungoma Samuel Kimiti kuingilia kati ili kukomesha ufisadi katika ofisi hiyo ya usajili wa stakabadhi hizo muhimu jambo ambalo litawasaidia wakaazi kupata usaidizi kwa haraka.
Hii hapa sauti ya mmoja wa wakaazi akielezea masaibu wanayopitia wanapotafuta usaidizi katika Ofisi hiyo
By Hillary Karungani