Viongozi wa kidini katika kaunti ya Kakamega wanaitaka serikali na viongozi kushirikiana kubuni mbinu za kukuza vipawa vya vijana ili kuepuka vifo kupitia kwa dawa za kulevya
Wakiongozwa na mchungaji Obadia Lumiti kwenye mazishi ya kijana Stephen Mwimali katika kijiji cha Ibale kata ndogo ya Indangalasia wamesema vijana wengi wamekuwa waraibu wa dawa za kulevya kwa kukosa usaidizi wa mwelekeo maishani
Wakazi wa eneo hilo wameunga mkono usemi huo wakisuta kituo kimoja cha ugemaji kwa kuwapotosha vijana
Kwa upande mwingine wachungaji hao wanaitaka serikali kuruhusu ibada za watu wachache kama ilivyoelekezwa na waziri
By Lindah Adhiambo