Hatua ya kuahirishwa uchaguzi wa bodi mpya kwenye chama cha ushirika cha kimabole eneobunge la Mlima Elgon imepokelewa vyema na wanachama huku wakimpongeza mkurugenzi wa vyama vya ushirika kaunti ya bungoma kwa kufwata sheria na kusitisha zoezi hilo.
Wakiongozwa na Edward Namulala na bi Dorice Muyala wanasema hatua hiyo huenda ikatoa nafasi kwa bodi ya chama hicho kuendelea na kesi iliyowasilishwa mahakamani ya kutaka shirika la Tropical na Sasini kuachilia pesa ambazo chama cha ushirika cha kimabole kinadaiwa kudai mashirika hayo.
Aidha wamempongeza mkurugenzi wa vyama vya ushirika kaunti ya Bungoma Stanslus Wambani kwa kile wanachosema kuwa na msimamo dhabiti kwa kufwata sheria za vyama vya ushirika kikamilifu.
Awali wambani alionyesha kushangazwa na hatua ya mkurugenzi wa vyama vya ushirika eneobunge la Mlima Elgnon Eric Kibet Kiso kwa kupendekeza kuandaliwa uchaguzi kwenye chama cha Kimabole akisema zoezi hilo halikufaa kuendeshwa.
By Imelda Lihavi