Brighton waipokeza Liverpool kichapo cha pili nyumbani kwao Anfield Steven alzate alifunga bao la kipekee katika mchezo huo kwenye awamu ya pili huku wana Liverpoool wakihangaika kubuni nafasi za mabao.

Liverpool kwa sasa wameshikilia nafasi ya nne wakiwa na pointi 40 alama saba kufikia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu iliyoshikiliwa na Manchester city.

 Bao hilo liliwapa nguvu Liverpool huku wakizindua mashambulizi wakitafuta bao la kusawazisha. Lakini safu ya ulinzi ya Brighton iliwatatiza vijana wa Klopp na kukaribia kufunga kupitia kombora la Mo Salah kutoka kwa Krosi ya Trent-Alexander Arnold lakini alipoteza nafasi hiyo.

Kikosi cha Graham Potter kilikuwa na nafasi nyingi za wazi lakini wenyeji walionekana kukaza katika mechi za nyumbani. Ushindi huo una maana kuwa Liverpool wamepoteza mechi tatu za nyumbani bila kufunga bao kwa miaka 36 baada ya kushiriki mechi 68 za awali bila kichapo ugani Anfield.

Man United wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 44, ikifuatiwa na Leicester City katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42 na Arsenali wakishikilia nafasi ya kumi na pointi 31.

Story by Austin Shambetsa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE