Bunge la kaunti ya Kakamega kwa kauli moja limeidhinisha mswada wa ripoti ya BBI na kuwa kaunti ya 13 kati kaunti zote 47 kuidhinisha mswada huo.
Ni wawilikishi wadi wawili tu kati ya 89 katika bunge hilo ambao walipinga mswada huo ambao uliwasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya haki na sheria bungeni humo Bornface Akosi.
Wengi wa wawakilishi hao wa wadi waliounga mkono mswada huo wanasema hatua ya kugatua raslimali zaidi mashinani ndio iliwachochea kuukumbatia.
Hata hivyo waliopinga mswada huo wakiwemo mwakilishi wa wadi ya Isukha Kusini Farouk Machanje, anasema kuna baadhi ya vipengee kwenye mswada huo ambavyo sio za kuwanufaisha wananchi wa kawaida.
Gavana Wycliffe Oparanya pamoja na seneta mteule Naomi Shiyonga ambao walihudhuria kikao hicho wamewapongeza wabunge hao kwa kuidhinisha mswada huo.
Story by Richard Milimu