Siku chache baada ya serikali ya kaunti ya Kakamega kuzuia mwili wa aliyekuwa afisa mkuu wa mifugo daktari Kelly Nelima kuzikwa kwenye shamba lake lililoko mtaa wa Kefinco viungani mwa mji wa Kakamega kwa madai kuwa ni ardhi ya Manispaa ya Kakamega, wenyeji wa wadi ya Shieywe wakiongozwa na mwenyekiti wa mafundi wa magari ambaye pia ni mwanasiasa Moses Musundi wametishia kuandamana ikiwa serikali ya kaunti hiyo haitabadilisha uamuzi huo.

Akiwahutubia waombelezaji kule Lurambi Musundi anasema kuwa ni makosa serikali kupiga marufuku wenyeji kuzika wapendwa wao kwenye ardhi za mababu wao akidai kuwa ardhi hizo sio ya serikali baali waliridhi kutoka kwa mababu zao.

Kulingana na Musundi anasema kuwa wana hati miliki za mashamba hayo na kuitaka serikali ya kaunti kusitisha uamuzi huo la sivyo waandae maandamano ya kupinga hatua hiyo.

Story by Imelda Lihavi

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE