Kaunti ya Kakamega imezidua chanjo ya korona hivi leo huku waziri wa afya katika kaunti hiyo Collins Matemba akiwa wa kwanza kudungwa chanjo hiyo.

Kaunti ya Kakamega imepokea  dosi 12,000  kwa jumla ya dosi 27,640 inayotarajia kutoka wizara ya afya. Aidha gavana Oparanya katika uzinduzi wa chanjo hiyo amesema chanjo hiyo itasaidia pakubwa katika kupigana na makali ya virusi vya korona na kuwahakikishia wananchi kuwa chanjo hiyo iko salama…..

Vilevile gavana Oparanya amedokeza kuwa katika awamu ya kwanza wataangazia sekta ya afya,  maafisa wa usama pamoja na taasisi ya elimu  huku akiwataka wahisani kujitokeza na kushirikiana na wahudumu wa afya katika kuihamasisha  jamii kuhusiana na chanjo hiyo……

Oparanya hata hivyo amesema kama kaunti wamejipanga kwa kukabiliana na wimbi la tatu linalokisiwa kuripotiwa nchini kwani wameongezwa vifaa hospitalini pamoja na wahudumu wa afya huku  akiwataka wananchi kuzingatia sheria za wizara afya ili kuzuia maambukizi zaidi.

Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE