Wito umetolewa kwa wizara ya kilimo katika serikali ya kaunti ya Bungoma kuweka mikakati itakayowasaidia wakulima kufufua kilimo cha pamba ili waweze kunufaika na kiwanda kipya kilichojengwa katika eneo la Malakisi eneobunge la Sirisia.

Akizungumza mjini Malakisi aliyekuwa diwani kwa wakati mmoja Nelson Okumu amesema wakulima wa zao la pamba wanatarajiwa kunufaika hata zaidi, baada ya kiwanda kipya cha pamba kujengwa eneo la Malakisi huku akitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Bungoma, kuwapa wakulima mbegu kama njia moja ya kukifufua kilimo cha pamba.

Aidha Okumu ameitaka serikali ya kitaifa kulikarabati daraja la Sango analosema linahatarisha maisha ya wakaazi. 

Wakati uo huo amelalamikia tatizo la ukosefu wa maji  eneo hilo licha ya kuwepo mradi wa kusafisha maji unaodaiwa kuwanufisha wakazi wa sehemu zingine.

By Hillary Karungani

.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE