Wakaazi wa kaunti ya Kakamega wateta kutokana na serikali ya kaunti kukosa kutekeleza miradi muhimu licha ya kutengewa fedha kila mwaka wa bajeti 12

Serikali ya kaunti ya Kakamega imetakiwa kuyapa maswala ya maji, uboreshaji wa miundo misingi na afya kipaumbele kwenye bajeti ya mwaka wa 2021/2022. Hii ni baada ya wakaazi wa kaunti hiyo kutoa malalamishi kwenye mkutano wa kutoa maoni kuhusu bajeti ya kaunti hiyo ya mwaka wa 2021/2022 kwamba miradi  muhimu imesalia kutokelezwa kikamilifu kila mwaka wao wakilisalia kutofaidika.

Ni maswala ambayo kulingana na mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Kakamega Willis Opuka akizungumza baada ya kikao hicho mjini Kakamega amesema kuwa kama bunge watahakikisha kwamba fedha ambazo zimetengewa miradi ya kunufaisha wananchi inatekelezwa ipasavyo bila kuingiliwa serikali ya kaunti


 Aidha mwenyekiti huyo alionekana kutetea hatua ya kutomalizika kwa mradi wa maji ambao ulianzishwa na serikali ya kaunti iliotengewa takribani shilingi milioni 50 katika eneo bunge la Khwisero na kufikia sasa haujakamilika licha ya kuanzishwa miaka mitatu iliyopita

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE