Naibu chifu wa kata ndogo ya Kakunga eneo la Malava kaunti ya Kakamega Jackson Wambulwa amewataka wakazi kuzingatia marufuku ya denzi za usiku kwenye hafla za matanga maarufu kama Disco Matanga
Akihutubu kwenye mazishi ya Samwel Chikwanyi kijiji cha Shianda, Wambulwa amesema Disco Matanga imeathiri jamii pakubwa hasa nidhamu ya vijana na ametangaza kuwachukulia hatua wamiliki wa mitambo iwapo watapatikana
Aidha Wambulwa amewataka wakazi ambao walisajili kadi za Huduma Namba katika wadi kata hiyo na wamehamia sehemu zingine kujitokeza na kuzichukua kwani imekuwa vigumu kuwapata
By Imelda Lihavi