Jumla watu 19 wameaga dunia tangu mwezi huu Juni uanze kutokana na janga la virusi vya korana katika kaunti ya Kakamega; haya ni kwa mjibu wa gavana wa kaunti hii Wycliffe Oparanya akitoa taafira kwa vyombo habari mjini humo

Gavana oparanya amesikitikia idadi ya watu ambao wameambukizwa virusi hivyo katika hii akisema kuwa kuna jumla ya wagonjwa ishirini ambao wamelezwa katika hospitali za kaunti hii wakiwemo wa kutoka kaunti jirani

Kutokana na mchemko wa virusi hivyo, gavana Oparanya ametawataka baadhi ya wafanyakazi wa kaunti hii kuanza kufanya kazi wakiwa nyumbani kwa muda wa siku kumi na nne na kulitaka bunge la kaunti hiyo kuhudhuria na theluthi tatu ya wakilishi wadi kama njia ya kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo

Oparanya hata hivyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya kuwepo kwa hewa safi aina ya oksijeni na kufichua tayari serikali yake imeagiza mtambo mpya kutoka nchi ya france ambao unatarajiwa kupiga jeki kwa uzalishaji wa hewa hiyo Kakamega

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE