Zaidi ya watu 7 wa familia moja kutoka kijiji cha Butali eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wamelazimika kukeshe nje ya nyumba yao baada ya maafisa wa usalama waliojihami kubomoa nyumba wanamoishi na kuaribu mali ya maelfu ya pesa
Akizungumza na kituo hiki nyumbani kwake mwathiriwa wa kisa hicho bi Susan Miches amehoji kuwa wanawe wamo hatarini wakupatwa na magonjwa yanayotokana na baridi hasa wakati huu wa mvua na kuiomba serikali kuingilia kati na kuwanusuru.
Kulingana na Miches Charles ambaye ni miongoni mwa waathiriwa amesema kuwa walikuwa wakizozana na nduguye kuhusiana na kipande hicho cha ardhi ambacho walipewa na baba yao ambacho kimesababisha kisa hicho.
Tumekua na mzozo kwa sababu ya shamba hii na nadhani ndio imepelekea kwa huu uvamizi na tukabomolewa nyumba
Selina charles ambaye ni mama mix charles amelaani kitendo hicho na kudai kuwa hawana stakabadhi za kumiliki shamba hilo ambazo zinaweza kupelekea kutoa agizo la mahakama ya kubomolewa nyumba zao.
Hata hivo kamanda wa polisi katika kituo cha police cha Kabras Peter Mwanzo ameeleza kuwa alichukuwa hatua hiyo baada ya kupokea agizo la mahakama kutekeleza ubomozi huo.