Eneobunge la Lurambi ndilo limefanya bora kaunti ya Kakamega katika mitihani ya kitaifa ya mwaka wa 2020 na hata kuhorodheshwa la tatu katika uliokuwa mkoa wa Magharibi
Akizungumza katika ziara yake kwa baadhi ya shule eneobunge la Lurambi, mbunge wa eneo hilo askofu Khamala amewapongeza walimu, washika dau, wanafunzi na wazazi kwa kuchangia kwa matokeo hayo bora na kuahidi kuwepo siku ya elimu ili kuwatuza waliotia fora
Khamala aliweza kuzuru shule za Matende, Bukhulunya na Emulele katika wadi za Butstso ya Kati na Shirere na Kufungua madarasa matatu katika shule ya Bukhulunya na kuahidi kuanzisha ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Emulele itakayogharimu kitita cha shilingi milioni 4.4 kutoka azina ya CDF
Walimu wa shule hizo hawakuficha furaha zao wakielezea masaibu ambayo yamekuwa yakiwakumba kutokana na uchache wa madarasa shuleni mwao.
Aidha mbunge huyo aliyehorodheswa nafasi ya thelathini na tano kote nchini kwa utenda kazi kutokana na orodha uliyotolewa hivi maajuzi amewataka wakaazi wa eneobunge la lurambi kumrejesha bungeni kwa awamu ya pili angaa aikamilishe miradi yake
By Richard Milimu