Mwakilishi wa Wadi ya Chesikaki Ben Kipkut ameombwa kushirikiana kwa karibu na idara ya maji katika serikali ya Kaunti ya Bungoma ili kulifaidi eneo la Chesikaki na maji safi ya kunywa.
Kwa mujibu wa msemaji wa watu wenye ulemavu Kaunti ya Bungoma Ben Obama, eneo la Chesikaki hadi sasa linakumbwa na tatizo la uhaba wa maji, hali inayowatatiza pakubwa wakazi.
Obama vile vile amelalamikia mgao wa fedha unaotolewa na serikali kuwafikia walemavu, akisema idadi kubwa ya walemavu mashinani hawajawahi kunufaika na fedha hizo.
Alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa walemavu eneo bunge la Mlima Elgon kwenye uhamasisho kuhusu mgao wa fedha za walemavu.
By Richard Milimu