Vuta nikuvute ilishuhudiwa katika kanisa la makao makuu ya Ebumamu Church of God yaliyoko eneo bunge la Butere kaunti ya Kakamega baada ya ibaada ya kumuapisha askofu mpya wa kanisa hilo Jackson Saya kusitishwa na serikali kwa madai ya kutofwata maagizo ya wizara ya afya kuthibiti ugonjwa wa covid 19.

Haya yalitokea baada ya chifu wa kata ya Marama ya Magharibi bi Martha Emitekho kusimamisha ibaada hiyo kwa kutumwa na naibu kamishona wa Butere kwa kupata fununu kuwa ibaada hiyo inaendelea pasina kufwata masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kuthibiti msambao wa virusi vya corona.

Waliohudhuria ibaada hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa bodi ya kanisa hilo Joshua Oulo walinyoshea kidole cha lawama aliyekuwa askofu wa kanisa hilo kwa muda wa miaka 11 James Akhungu kwa madai ya kutokubali kushindwa kwenye uchaguzi huku walimsuta kwa kulitenganisha dhehebu hilo na kulirudisha nyuma kimaendeleo.

Hata hivyo shughuli hiyo iliendelezwa katika kanisa la Emahongoyo lililoko katika wadi ya Marenyo/Shianda chini ya askofu mkuu wa kanisa hilo nchini Walter Liatema  huku askofu Jackson Saya akiapishwa rasmi na kukisuta kitendo hicho na kuwakikishia waumini kuwa atasuluhisha migogoro ya uongozi inayozidi kushuhudiwa kila wakati.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE