Kampuni ya Kenya Power mjini Bungoma imepewa ilani ya siku thelathini kufidia familia moja eneo la Nalondo eneobunge la Kabuchai baada ya nyaya za stima zilizokuwa zikining’inia kudaiwa kukatiza maisha ya mpendwa wao hivi maajuzi.
Akiwahutubia wanahabari eneo la Nalondo mwanaharakati wa kisiasa eneobunge la Kabuchai, Evans Kakai anasema tangu tukio ambapo mkaazi mmoja anadaiwa kuangukiwa na nyaya za stima na kupelekea mauti yake bado usimamizi wa kampuni hiyo haujatoa taarifa yoyote kuhusu kisa hicho.
Wakati uo huo Kakai amewataka wabunge katika bunge la seneti na lile la kitaifa kuhakikisha wanajadili na kupiga msasa ripoti ya BBI kwa kina kablaya kuiwasilisha kwa wananchi kuamua iwapo wataiunga mkono au la.
Kadhalika ametoa wito kwa serikali kuweka mikakati kabambe itakayosaidia kuimarisha uchumu ambao umeonekana kudorora kufwatia mkurupuko wa janga la corona.
By Hillary Karungani