Familia moja kutoka kijiji cha Block Ten mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu inaomba msaada baada ya kubarikiwa na watoto watatu.
Kulingana na Mohammed Mulati ambaye anajulikana kama mustafa amekiri kuwa amekuwa na changamoto ya kulea familia yake hasa tangu mkewe kujifungua na kwa sasa akiwa na watoto sita, wawili wakiwa shuleni.
Mustafa amesihi kuwa bali na kuwa na changamoto ya kupata lishe pia mwenye nyumba amempa ilani ya kuhama na hana mahali pa kuenda na imekuwa ni vigumu kupata ajira.
Mustafa ameomba wahisani kuingilia kati na kumsaidia hata angalau kazi ambayo atajikimu kimaisha.
Story by Sharon Lukorito