Viongozi wa kanisa la Landmark linalopatikana katika kijiji cha Chepchori katika wadi ya Sang’alo-Keplonik eneo bunge la Mosop kaunti ya Nandi, wameachwa katika hali ya mshangao baada ya mchungaji wao kubomoa na kung’oa milango na madirisha ya kanisa hilo.
Wakizungumza na kituo hiki cha 102.2 lubao fm, viongozi hao wanasema kwamba chanzo cha kufikia ubomozi wa kanisa hilo ni baada ya mchungaji wao kubadilisha jina la kanisa kwa mara kadhaa.
Mweka hazina wa kanisa hilo Bi. Emily Ng’etich anasema kwamba wameshangaa sana kupata mchungaji amebomoa kanisa na kuchukua kila kitu huku akiwa na lengo la kurudi kuuza kiwanja cha kanisa.
Hata hivyo, mkewe mchungaji huyo kwa jina Jane Eleko Mashati ambaye ndiye mke wa kwanza anatoa wito wa kusaidia kiwanja kisiuzwe na mmewe.
Story by Sajida Wycliffe