Watu watatu kutoka familia moja akiwemo mama , baba na mtoto msichana wa miaka mitatu wanauguza majeraha mabaya katika hospitali ya misheni ya Ingotse baada ya kupigwa na radi nyumbani kwao katika kijiji cha Emachembe wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi.

Wakizungumza wakiwa kwenye wadi kwenye hospitali ya misheni ya Ingotse, waasiriwa hao wakiongozwa na dorine amboka wa miaka 34 na mumewe  Gilbert Amboka wa miaka 36  wanasema kuwa walikumbana na kisa hicho walipokuwa nyumbani mwao wakati wa jioni mvua ilipokuwa ikinyesha.

Wakati uo huo waathiriwa hao wameitaka serikali kuingilia kati kuwawekea mashine ya kunasa radi maeneo hayo kuzuia visa sawia. 

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE