Mshukiwa mmoja wa uhalifu ameuawa kwa kuteketezwa na wananchi kwa tuhuma za kuwaiba kuku na sufuria kwenye boma la mkazi mmoja katika kijiji cha Sossian kata ndogo ya mwamba eneo bunge la Lugari  kaunti ya Kakamega.

Akithibitisha kisa hiki OCPD wa Lugari  Bernard Ngungu amesema mwendazake Francis Mutuve, aliingia bomani mwa Harrison Shairo Mwendo wa saa tisa usiku na kuiba kuku,sufuria na sahani ,kabla ya mwenye boma hilo kumsikia na kupiga mayowe, yaliyowavutia majirani, walioamka na kufanikiwa kumshika mshukiwa, na kumkatakata kabla ya kumteketeza.

Inaarifiwa kuwa mshukiwa  huyo aliyekuwa amejihami kwa upanga, anaodaiwa  kutumia  kumkata na kujeruhiwa mmoja wa wanawe Shairo kabla ya kuuawa.

Aidha Ngungu amewaonya wananchi dhidi ya kujichukulia sheria mikononi mwao, huku akiwataka  wananchi  kuwakabidhi washukiwa kwa mafisa polisi ,ili hatua ifaayo kisheria iweze kuchukuliwa dhidi yao.

Maiti yake ya mwendazake  iliondolewa na kupelekwa katika makafani ya  kimbilio  Kipkaren, huku uchunguzi  wa kina ukianzishwa kuhusiana na kisa hiki.

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE