Familia ya marehemu Timothy Muleko Shienji aliyeaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani majumaa kadhaa yaliyopita kutoka kijiji cha Mukhuyu,lokesheni ndogo ya Lubao,wadi ya Isukha Kazkazini,eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega imeirai serikali ya kaunti ya Kakamega chini ya gavana Wycliffe Ambetsa Oparanya kuingilia kati na kuwasaidia kumudu gharama ya matibabu ya marehemu ambayo kwa sasa ni shilingi elfu mia moja tisini
Kabla ya kifo chake marehemu amehudumu kama muhudumu wa bodaboda katika steji ya okumu mita chache kutoka soko la Lubao na kuwacha masaibu si haba kwenye familia yake
Bibiye marehemu kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya Kakamega baada ya kujifungua huku familia hiyo ikizidi kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ada za juu za hospitali hiyo kando na kuwa marehemu ameacha watoto ambao wawili wapo katika shule za upili Bukhaywa na Mtakatifu Monika iliyoko Lubao
Ni maoni yalioungwa mkono na nduguye marehemu Jethro Ihachi kwa kuiomba serikali ya kaunti ya Kakamega na wahisani kujitokeza na kusaidia familia hiyo
Naye msimamizi wa kikundi cha nduru welfare Caleb Imboyoka Kaburu kikundi kinachowasaidia wanakijiji wa sehemu hizo wanapopatwa na msiba pia akiitaka serikali ya kaunti kusaidia familia hiyo kwani mchango wa kikundi hicho huwezi kufikia ada zilizowekwa na hospitali ya rufaa ya Kakamega
Naye mwenyekiti wa bodaboda katika steji ya okumu Samuel Musotsi akitilia mkazo kwa semi hizo na kutaka wahisani kujitokeza kusaidia familia ya mmoja wao
By Javan Sajida