Familia moja ya watu tatu kutoka kijiji cha Musese eneobunge la Kabuchai inaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Chwele baada ya kudaiwa kula uyoga uliotolewa msituni ukiwa wenye sumu.

Kulingana na biEeunice Majimbo ilikuwa siku ya Jumatano juma hili mwendo wa saa tatu asubuhi ambapo mwanawe mdogo alirejea nyumbani na uyoga na baada ya kuutayarisha kisha kisha familia yake kula ndipo walianza kuhisi maumivu ya tumbo baada ya masaa mawili.

Aidha wanasema kwa sasa wanaendelea kupokea nafuu baada ya kupokea matibabu katika hospitali hiyo ya kaunti ndogo ya Chwele.

Muuguzi mguu katika hospitali hiyo bi Eeverlyne Kusimba amewashauri wananchi kuwa waangalifu na vyakula hasa vinanavyotolewa msituni akisema huenda vikadhuru afya yao.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE