Huku wanafunzi na wazazi wakiendelea kusherekea matokeo ya wanao wa darasa la nane ambayo walitangazwa hapo jana na waziri wa elimu profesa george magoha, shule ya mingi ya kibinafsi ya fesbeth mjini kakamega imesalia kileleni mwa shule za kaunti hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa kwa kuandishi alama ya jumla ya mia 397.2 na kuipiku shule ya st. Peters mumias yenye jumla ya 391, hill school ya kakamega 386, booker academy 376 na shule msingi ya kakamega ambayo ilikuwa na jumla ya alama ya 345
Licha ya shule hiyo kuwa na mwanafunzi wa kwanza ryan prince na alama ya 421, nyuma ya wanafunzi wa st.peters mumias mark joe na oliver shema ambao walipata alama ya 427, na yule wa shule ya msingi ya kakamega emmanuel changulo ambaye alipata alama ya 426, mkurugenzi wa shule hiyo ruth minish amesema kuwa matokeo hayo ya kuridhisha yametokana na bidii ya wanafunzi na walimu mbali na kuwepo ushirikiano mwema na washika dau wote
Hata hivyo mkurugenzi huyo ametilia shaka jinsi shule za umma zilizipiku shule za kibinafsi kwenye mtihani huo akidokeza kuwa huenda kulikuwepo na njama fiche kwenye matokeo hayo ya shule za kibinafsi
By Richard Milimu