Huku mtihani wa kidato cha nne ukielekea kukamilika onyo kali imezidi kutolewa kwa wasimamizi wa mtihani watakao patikana wakiendeleza wizi wa mtihani huo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria
Haya ni kwa mujibu wa waziri wa elimu profesa gorge magoha akizungumza katika shule ya upili ya wavulana ya Kakamega alikozuru kutathmini jinsi mtihani huo unavyoendelea akisema hatua kali itachukuliwa kwa atakayehusika kwa udanganyifu huo.
Aidha karatasi hizo zinatarajiwa kuanza kusahihishwa wiki ijayo punde tu ya mtihani huo kukamilika.
Hata hivyo Magoha amewataka wasimamizi wa shule kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kudhibiti janga la Korona shule zitakapo fungunguka mwezi ujao.
By Richard Milimu