Familia moja kutoka  kijiji cha  Mahanga Webuye  yalilia haki baada ya  mwanafamilia wao ambaye ni mzee  mwenye umri wa miaka 49 John Nabiswa Masibo kudaiwa  kuaga dunia alipoingia katika jengo la Shiv Plaza mkabala  na kanisa katoliki la Chist The King  linaloaminika  kumilikiwa  na mhindi kwa jina Shiv na kuanguka chini kutoka Orofa ya tatu na kuaga papo hapo.

Kulingana na familia hiyo wanasema kwamba mpendwa wao alikua ameenda kuona wakili katika jengo hilo akiwa ameambatana na mwenzake ili kushughulikiua kesi ya mwanawe alipoingia katika chumba kimoja kwenye jengo hilo orofa ya tatu aliweza kuanguka chini na kuaga dunia.

Hata hivyo familia hiyo imelekeza lawama kwa wale wanaosimamia ubora wa majengo kaunti ya bungoma pamoja na mmiliki wa jengo hilo kwa kuacha sehemu hiyo wazi bila kueka ilani yeyote huku jengo hilo likasababisha maafa ya mpendwa wao.

Huku wakisisitiza mpendwa wao hangeweza kuaga dunia iwapo sehemu hiyo ingewekwa ilani 

Mwili wa mwendazake uliweza kufanyiwa upasuaji hapo jana katika hospitali ya rufaa ya Bungoma huku mmiliki wa jengo hilo bw Shiv akidinda kuongea na wandishi wa habari akielezea anakazi mingi anayoshughulikia na hana wakati wakuelezea yaliojiri Swali ni Je  ni nani atakaye sadia familia hiyo kupata haki?

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE