Wakenya wametakiwa kuzingatia kilimo wakati huu taifa linapokaribia kwenye uchaguzi mkuu ujao 2022
Ni kauli yake naibu chifu wa lokesheni ndogo ya lubao sulvei shiafu ashiono akihutubia waombolezaji kwenye ibaada ya maombi na mazishi ya mama robai namisoho james katika kijiji cha handidi mapema hii leo
Sulvei amesema hilo litasaidia kumaliza njaa na mahangaiko ya kutafuta pesa kwa wanasiasa wakati wa uchaguzi mkuu unapo karibia
Wakati uo huo sulvei amewaonya wagemaji wa pombe aina ya chang’aa eneo la Ikhamala na kuwaahidi kuwa mkono wa sheria utawafikia na kuharibu vituo viwili vinanyo haribu maisha ya wakaazi eneo hilo la Handidi
By Sajida Javan