Kamati ya ugatuzi na fedha imeandaa kikao kupokea ripoti kuhusu kusimamishwa kwa bajeti ya kaunti ya Vihiga baada ya wakazi wawili Joseph Simekha na Francis Ominde kuwasilisha kesi mahakamani na bunge la seneti wakipinga makadrio ya bajeti ya mwaka 2021/2022 wakidai bunge la Vihiga lilipitisha bajeti hiyo pasina ya kuhusisha wananchi.

Akiongea kwenye kikao hicho mwenyekiti wa kamati hiyo seneta Rose Nyambunga, seneta wa Kakamega Cleophas Malala na seneta mteule bi. Halima Abdille, kwa pamoja walitaka pande zote kutanzua migogoro yao ili kutoa nafasi kwa wanachi kupokea huduma, na hata kuondoa kesi hiyo mahakamani.

Katika kikao hicho naibu gavana wa Vihiga Patrick Saisi alimshtumu gavana wake dkt. Wilbur Otichillo kumtelekeza katika shughuli zote za kiserikali na hata kukosa mshahara wake kwa muda.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE