Kinara wa chama cha Amani National Congress ANC Wycliffe Musalia Mudavadi amekamilisha ziara yake ya siku mbili kaunti ya Nyandurua hii leo baada ya kuhudhuria hafla ya kanisa katika dhehebu la mtakatifu Cecillia huko Milangine, dhehebu la Apostolic Faith sehemu za Njabi-in na katika hafla za kukutana na wakazi wa sehemu hizo 

Mudavadi amewarai wenyeji wa kaunti hiyo kuzingatia swala la amani kwenye uchaguzi mkuu ujao ili kutoliweka taifa kwenye misingi ya kikabila

Hata hivyo Mudavadi amewarai wenyeji kumuunga mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao ili kufufua uchumi wa taifa hili unaoendelea kutokota kila uchao

Mudavadi amesisitiza uchaguzi mkuu ujao utaandaliwa kama ilivyoratibiwa na kutaraji rais Uhuru Kenyatta ataondoka madarakani wakati huo

Akizungumza kwenye ziara hiyo seneta wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amepuuzilia mbali siasa zinazoenezwa na mrengo wa naibu rais William Ruto kama za kuwahadaa wakenya kwa kuahidi kushughulikia uchumi kwanzia chini hadi juu

Mudavadi aliandamana na gavana wa kaunti hiyo Francis Kimemia miongoni mwa viongozi wengineo 

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE