Chama cha Jubilee kimepata pigo baada ya baadhi ya viongozi na wanachama wake katika eneo bunge la Mumias Mashariki kutangaza kukigura chama hicho na kujiunga na chama cha ANC.

Wakiongozwa na katibu wa chama cha Jubilee katika eneo bunge la Mumias Mashariki Everlyne Awour, wamesema wameafiki uamuzi licha ya shinikizo za kuwataka kujiunga na chama cha UDA.

Usemi wao unajiri majuma mawili tu baada ya afisi za chama cha Jubilee katika kituo cha kibiashara cha Shianda kupakwa rangi na kuchorwa nembo ya chama cha UDA.

Kwa kauli moja wamemsuta mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali kwa kile walichosema ni kuwatelekeza licha ya wao kufanya kila wawezalo kuona kuwa amehifadhi kiti hicho.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE